BUNGE LA TRANS NZOIA LAAHIDI KUSHUGHULIKIA WAFANYIBIASHARA WALIOBOMOLEWA VIBANDA.


Wafanyibiashara walioathirika na ubomozi wa vibanda mjini Kitale katika kaunti ya Trans nzoia wametakiwa kutayarisha malalamishi yao na kuyawasilisha katika bunge hilo.
Ni wito wake spika wa bunge hilo Joshua Werunga baada ya wafanyibishara hao kulitaka bunge hilo kuingilia kati masaibu wanayopitia kufuatia kuathiriwa biashara zao.
Werunga amesema kuwa bunge hilo litabuni kamati itakayoshughulikia malalamishi ya wafanyibiashara hao kwa kuzingatia sheria na kuandaa mapendekezo yake ili kuhakikisha kuwa wafanyibiashara hao wanapata haki.