BUNGE LA TAIFA LALAUMIWA KWA ONGEZEKO LA BEI ZA MAFUTA YA PETROLI.


Baadhi ya wahudumu wa boda boda katika kaunti hii ya Pokot magharibi sasa wameelekeza ghadahabu zao kwa bunge la taifa kwa kutochukua hatua za kuhakikisha bei ya mafuta inadhibitiwa nchini baada ya mamlaka ya kudhibiti bei za bidhaa za mafuta nchini EPRA kutangaza ongezeko la bidhaa za petroli.
Wakizungumza mjini makutano wahudumu hao wamesema kuwa bunge la taifa ndilo lililo na uwezo wa kubuni sheria za kudhibiti ongezeko la bidhaa za mafuta nchini na hatua ya kuruhusu kupandishwa bei za mafuta kiholela nchini inaashiria kuwa halimjali mkenya wa kawaida.
Wahudumu hao wameishutumu serikali kwa kile wamedai kuendeleza ukatili dhidi ya wakenya hasa baada ya serikali yenyewe kutangaza njaa kuwa janga la taifa kwa baadhi ya kaunti nchini hali ambayo ilifaa kuifanya kuhakikisha bei za bidhaa zinapunguzwa ili kuwanusuru wakenya.
Wamesema ongezeko hilo la bei za mafuta litaathiri zaidi hasa sekta ya boda boda ikizingatiwa kazi katika sekta hiyo imerudi chini mno.