BUNGE LA POKOT MAGHARIBI LAJITETEA KUHUSU HATUA YA KUMTIMUA SPIKA.
Baadhi ya waakilishi wadi kaunti hii ya pokot magharibi hasa waliochangia hoja ya kumbandua spika wa bunge la kaunti hii Catherine Mukenyang wamevunja kimya chao kutokana na shutuma ambazo zinaelekezwa dhidi yao kufuatia hatua hiyo.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Kodich Philip Palor, viongozi hao wamekanusha vikali madai kuwa walihongwa na baadhi ya viongozi katika kaunti hii ili kumbandua mukenyang wakisema kuwa ziara zao maeneo mbali mbali ya nchi kabla ya kikao cha kumbandua Mukenyang zilikuwa za kikazi wala hazikuhusu kwa vyovyote hatua hiyo.
Palor amesema kuwa Mukenyang alitimuliwa kufuatia mienendo yake ambayo ilikwenda kinyume na matarajio, akidokeza kuwa kabla ya kutimuliwa kwake yapo majaribio mengine matatu ambayo yalikusudiwa kumwondoa afisini ila akawa anapewa muda wa kurekebisha mienendo yake swala ambalo hakulifanya na kumpelekea kubanduliwa afisini.