BUNGE LA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KUSHIRIKI KIKAO CHA DHARURA CHA KUJADILI BAJETI YA ZIADA YA MWAKA WA 2020/21


Bunge la kaunti ya Pokot Magharibi linatarajiwa kuandaa kikao spesheli cha dharura leo hii ili kuweza kujadili bajeti ya ziada ya kaunti hii ya mwaka wa 2020/2021
Hata hivyo Kalya Radio imebaini kwamba gavana Lonyangapuo na spika Catherine Mkenyang walikuwa na mkutano wa faraghani katika makao makuu ya gavana uko Kapenguria hiyo jana mkutano ambao ulichukua masaa matano kujadili maswala kadhaa huku wakimnyoshea kidole cha lawama waziri wa fedha kaunti hii ya Pokot Magharibi Christine Apakoreng kwa kukiuka makubaliano yao.
Ikumbukwe awali spika wa bunge la kaunty ya Pokot Magharibi Catherine Mukenyang alikuwa amesitisha kikao hicho maalum cha kujadili bajeti ya ziada ya kaunti hii mwaka wa 2020/21 iliyotarajiwa kufanyika hiyo jana hatua iliyoonekana kubainisha ubabe wakisiasa kati yake na gavana Lonyangapuo.
Katika waraka kwa wawakilishi wa wadi spika Mukenyang alikuwa amefutilia mbali kikao cha leo akidai kuwa waziri wa fedha Christine Apakoreng alikiuka makubaliano kati ya gavana Proff John Lonyangapuo na bunge la kaunti hiyo kuhusu maswala kadhaa yakiwemo kucheleweshwa kwa mishahara ya wawakilishi wa wadi na wafanyikazi wa bunge.
Kalya Radio imebaini kwamba bunge hilo la Pokot Magharibi lilifaa kuelekea mapumuzikoni hadi tarehe tisa Februari mwaka ujao swala ambalo halijabadlishwa.