BUNGE LA KAUNTI POKOT MAGHARIBI LAOMBOLEZA KIFO CHA KIONGOZI WA WENGI.


Bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi limemwomboleza aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge hilo Thomas Ng’olesia.
Akituma risala za rambi rambi kwa niaba ya bunge hilo, Spika Catherine Mukenyanga amemtaja Ng’olesia ambaye pia alikuwa mwakilishi wadi wa Seker kuwa kiongozi shupavu ambaye alipigia upatu zaidi demokrasia na haki za kibinadam.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Mukenya amesema kuwa bunge hilo litamkosa pakubwa Ng’olesia kutokana na michango yake ya busara bungeni na uongozi ambao haungepigiwa mfano.
Amesema mipango ya mazishi ya mwenda zake itatangazwa baadaye.