BUNGE LA BUNGOMA KUREJELEA VIKAO JUMA LIJALO BAADA YA KUFUNGWA KWA MUDA.


Bunge la kaunti ya Bungoma litaanza kujadili mswada wa bajeti wa mwaka 2021/2022 kuanzia wiki ijayo.
Kiongozi wa wengi katika bunge hilo Joseph Nyongesa amesema kuwa bunge hilo litajadili mswada huo bila kushurutishwa na sehemu ya waakilishi wadi ambao waliandamana nje ya bunge hilo siku ya jumatano juma hili.
Naibu spika wa bunge hilo Stephen wamalwa amekosoa vikali vurugu ambazo zilisababishwa na baadhi ya waakilishi wadi nje ya bunge hilo wakimshinikiza spika Emmanuel Situma kufungua bunge ili wajadili na kupitisha mswada huo wa bajeti.