BIASHARA YA WATOTO YAKITHIRI MAPAKANI PA KENYA NA UGANDA
Visa vya dhuluma dhidi ya watoto vimeongezeka maeneo kadhaa katika taifa jirani la Uganda hasa baada ya shule kufungwa kote nchini humo kufuatia kuongezeka kwa maambukizi ya virus vya corona.
Akizungumza huko amudat mpakani pa kaunti hii ya pokot magharibi na taifa jirani la Uganda naibu mshirikishi wa kitaifa katika idara ya kuzuia biashara ya watoto Agnes Ekoye, amesema kuwa biashara ya watoto imeripotiwa kuongezeka hasa eneo la karamoja ambapo wanaingizwa nchini Kenya hadi Somalia.
Ekoye ameyasema hayo baada ya kikao na wadau huko Amudat kutathmini mikakati ambayo itawekwa kukabili visa hivi, ambapo pia amesema kuwa wengi wa watoto hawa hasa wa kike wamekuwa wakidhulumiwa pakubwa kingono.