BI. HARUSI WA “ROHO MTAKATIFU” AAGA DUNIA.


Mkazi mmoja wa kaunti hii ya Pokot magharibi aliyegonga vichwa vya habari mwaka jana kwa kudai kufunga harusi na roho mtakatifu amepatikana amefariki katika hali isiyoeleweka.
Kulingana na Jackson kapatet ambaye ni askari wa kaunti aliyekuwa akifanya kazi na mwenda zake, Elizabeth Nalem aliondoka nyumbani kwake majuma matatu yaliyopita bila taarifa kabla ya mwili wake kupatikana msituni ukiwa tayari umeoza ambapo inakisiwa huenda alivamiwa na wanyama wa mwituni.
Ni kisa ambacho kimethibitishwa na OCPD wa Kapenguria Kipkemoi Kirui ambaye amesema polisi wanatarajiwa kuanzisha uchunguzi ili kubaini kilichopelekea kifo cha mwenda zake.
Ni mwaka jana ambapo marehemu aligonga vichwa vya habari baada ya kudai kuagizwa na Mungu kufanya harusi na roho mtakatifu ili kuanza rasmi kufanya kazi yake tukio liliwashangaza wakazi wengi wa kaunti hii.