BBI KUWANUFAISHA WALIMU WANAOISHI NA ULEMAVU BUNGOMA


Walimu zaidi wa chekechea wenye ulemavu wataajiriwa baada ya mswada wa marekebisho ya katiba ya mwaka 2020 kupitishwa.
Haya ni kulingana na serikali ya kaunti ya Bungoma.
Akizungumza kwenye hafla ambayo aliongoza kwenye maeneo ya mabanda eneo bunge la Kanduhi gavana wa kaunti hiyo Wycliffe Wangamati amesema kuwa kuna nafasi 116 na silimia 30 zitawaendea wenye ulemavu, akina mama na hata vijana.
Naye waziri wa michezo kwenye kaunit hiyo Catherine Kakai amepongeza juhudi za gavana Wangamati kuangazia maslahi ya wale ambao wanaishi na ulemavu huku akitaka watu hao watengewe nafasi zaidi ndani ya wizara yake.