BARAZA LA WANAHABARI LAKUTANA NA WANAHABARI POKOT MAGHARIBI KUHUSU UCHAGUZI MKUU UJAO.


Baraza la wanahabari nchini limeandaa kikao na wanahabari wa kaunti hii ya pokot magharibi kuhusu utendakazi wao msimu huu wa siasa za uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Akizungumza baada ya kikao hicho mratibu wa baraza hilo kanda ya bonde la ufa Jackson Karanja amesema kikao hicho kilihusu kuwahimiza wanahabari kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili ya uanahabari wakati huu.
Aidha Karanja ametoa wito kwa wanahabari kuhakikisha wanawasilisha habari zenye usawa na zinazoheshimu maoni ya kila mmoja, pamoja na kuwa makini na wanachowasilisha ili vyombo vya habari visiwe chanzo cha uchochezi miongoni mwa jamii.