BARAZA LA MAWAZIRI LA RAIS WILLIAM RUTO LAENDELEA KUIBUA HISIA NCHINI.
Hisia mseto zimeanza kuibuliwa miongoni mwa wananchi kufuatia hatua ya rais William Ruto kuteua baraza lake la mawaziri.
Baadhi ya wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wamepongeza baraza hilo wakisema kuwa limezingatia usawa wa jinsia pamoja na usawa wa kimaeneo japo wakilalamikia kuachwa nje baadhi ya viongozi wa chama cha UDA wanaodai kuwa walistahili kutuzwa baada ya kupigania chama hicho zaidi.
“Hilo baraza la mawaziri liko sawa ila kuna baadhi ya watu ambao nilitarajia kuwaona katika baraza hilo ila sijawaona. Tunaomba serikali kuu izingatie sana waliosimama na chama kuanzia mwanzo hadi mwisho.” Walisema.
Wakati uo huo wakazi hao wamewataka mawaziri walioteuliwa katika baraza hilo kuhakikisha kubwa wanatoa kipaumbele kwa huduma kwa mwananchi, wakipendekeza yeyote ambaye hatawajibika katika utendakazi kuachishwa kazi na wengine kupewa fursa hiyo.
“Mawaziri waliochaguliwa katika baraza hilo wafanye kazi. Kwa sababu sasa Kenya inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi. Wasifike huko na kuanza tu kunywa chai kwenye afisi zao.” Walisema.
Katika baraza hilo, rais Ruto alimteua kinara wa Anc Musalia Mudavadi kuwa waziri mwenye mamlaka, aliyekuwa spika wa bunge la kitaifa Justine muturi kama mwanasheria mkuu na mercy wanjau kama katibu katika baraza la mawaziri.
Aidha waziri wa usalama wa kitaifa atakuwa prof. kithure kindiki, waziri wa fedha prof njuguna ndung’u ambaye hapo awali alikuwa gavana wa benki kuu nchini
Waziri wa utumishi wa umma atakuwa Aisha jumwa waziri wa ulinzi Aden duale, waziri wa maji Alice wahome waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Alfred mutual.
Waziri wa biashara ustawi wa viwanda atakuwa Moses kuria waziri wa jumuia ya Africa mashariki na sehemu kame na maeneo Rebecca miano waziri wa barabara na uchukuzi ni kipchumba murkomen waziri wa mazingira atakuwa roseline soipan tuya.
Waziri wa ardhi na ujenzi atakuwa zacharia mwangi , waziri wa utalii na wanyamapori pamoja na toradhi za kitaifa atakuwa penina malonza huku waziri wa kilimo akiwa mithinka linturi.
Waziri wa afya ni dkt susan nakhumicha wafula waziri wa habari na mawasiliano na maswala ya kidijitali ni Eliud owalo huku waziri wa elimu akiteuliwa kuwa Ezekiel machogu.
Waziri wa kawi amependekezwa Davies chirchir huku waziri wa maswala ya vijana na michezo Ababu Namwamba waziri wa ustawi na vyama vya ushirika Simon chelugui na waziri wa maswala ya madini ni Salim mvurya, waziri wa labour Florence Bore miongoni mwa wengine.
Rais Ruto pia amemteua monica juma kama mshauri wa maswala ya usalama wa kitaifa huku Harriet chigai akiteuliwa kuwa mshauri mkuu wa maswala ya haki za wanawake wote.
Wakati uo huo ametoa agizo la kuchapishwa kwa majukumu ya naibu wake rigathe gachagwa.
Katika tangazo hilo rais Ruto ametangaza kwamba Gachagwa atakuwa na majukumu kadhaa ya kuongoza mikutano ya baraza la mawaziri kusimamia mageuzi katika sekta ya umma kubuni na kuzifanikisha sera za serkali miongoni mwa majukumu mengine atakayopewa na rais.