BAJETI YA YATTANI YAKOSOLEWA NA MASHIRIKA YA KIJAMII


Mashirika ya kutetea haki za kibinadumu Kaunti ya Trans Nzoia yamekosoa bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha Ukur Yatani wakisema bajeti hiyo imekosa kuangazia matakwa ya wakenya wengi.
Wakiongozwa na Kefa Were wametaja bajeti hiyo kama kejeli kwa wakenya kwani kwa sasa wakenya wanapitia hali mgumu ya kiuchumi ikizingatiwa ukosefu wa mafuta na vyakula na hata maziwa kwenye maduka ya humu nchini.
Wakati huo huo Were amesema taifa la Kenya halina fedha za kutekeleza bajeti hiyo ya shilingi Trillioni 3.3, akisema italazimu Kenya kuendelea kuomba madeni zaidi ili kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye bajeti hiyo jambo ambalo amesema huenda likahujumu zaidi uchumi wa wakenya.