‘BABA’ KUZURU WANAWE WAWILI POKOT MAGHARIBI.


Mgombea urais wa chama cha muungano wa azimio la umoja one Kenya Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua wanatarajiwa leo kuzuru kaunti hii ya Pokot magharibi kuendeleza kampeni za muungano huo katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono wa wakazi wa kaunti hii.
Raila na msafara wake wanatarajiwa kuanzia kampeni zao eneo la chepareria na kisha Lomut.
Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi ambaye analenga kutetea kiti hicho Samwel Poghisio ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kujitokeza kwa wingi na kumkaribisha Raila na pia kumuunga mkono mwezi agosti ili apite katika duru ya kwanza.
Wito kama huo pia ulitolewa mapema juma hili na gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo anayenuia kutetea kiti hicho kupitia chama cha Kenya National Union Party (KUP) ambacho ni chama cha tanzu cha muungano wa azimio la umoja one Kenya unaoongozwa na Raila Odinga.
Hiyo jumatano wiki hii Raila na kikosi chake walikuwa kaunti ya Turkana ambapo aliendelea kukosoa manifesto ya mshindani wake wa UDA William Ruto akisema kuwa imepitwa na wakati huku akikariri kuwa ana mpango bora zaidi wa kuinua uchumi wa Kenya tofauti na Ruto.