BAADHI YA VITUO VYA POLISI KUHAMISHWA TIATI, BARINGO.

Na Benson Aswani
Serikali itahamisha baadhi ya vituo vya polisi katika eneo bunge la Tiati kaunti ya Baringo kama mojawapo ya hatua za kukabiliana na visa vya uhalifu eneo hilo.
Mshirikishi wa bonde la ufa George Natembeya amesema kuwa vipo baadhi ya vituo vya polisi ambavyo vimejengwa maeneo ambako hakuna uhalifu hali hamna kituo chochote sehemu ambako kunaripotiwa uhalifu wa mara kwa mara katika eneo hilo la Tiati.
Natembeya amesema kuwa Tiati ilikuwa maficho makuu ya wahalifu ambao wanatakeleza uhalifu wao katike bonde la Kerio na kuwa serikali itachukua hatua madhubuti za kuimarisha usalama katika eneo hilo.