BAADHI YA VIONGOZI TRANS NZOIA WAPUUZA MIITO YA KUPATANISHWA RAIS NA NAIBU WAKE.


Hisia mseto zimeendelea kuibuka nchini kufuatia tangazo la baraza la maaskofu wa kanisa katoliki kuwa lipo tayari kuwaunganisha rais Uhuru kenyatta na naibu wake William Ruto.
Wa hivi punde kuzungumzia swala hilo ni mwanasiasa chipukizi katika kaunti ya Trans nzoia Eric Simatwa ambaye amesema kuwa baraza la maaskofu linafaa kuangazia jinsi ya kushinikiza serikali kuwatumikia wananchi ipasavyo badala ya kuwaunganisha wanasiasa wenye mitazamo tofauti.
Ikumbukwe tayari Ruto amesema yuko tayari kufanya mazungumzo ya kupatanishwa na rais Kenyatta ili kutatua tofauti baina yao akidai kuwa waliochochea uhasama huo ni watu fulani wanaolenga kujinufaisha serikalini.