BAADHI YA VIONGOZI KAUNTI YA TRANSNZOIA WAMEWATAKA WENZAO KUKOMA KUKASHIFU UTENDAKAZI WA GAVANA ANAYEONDOKA PATRICK KHAEMBA


Wito umetolewa kwa wanasiasa wanaokosoa uongozi wa Gavana Patrick Khaemba katika mikutano zao za kisiasa badala ya kuuza sera zao kwa wananchi watakao wapigia kura.
Wakiongozwa na Mwakilishi wadi ya Tuwani Bernard Daddy Wambua amewataka wanasiasa hao kuelezea umma mambo watakao watekelezea iwapo watachaguliwa na kukoma kuzungumzia miradi ya maendeleo anayotekeleza kwa sasa.
Wakati huo huo Wambua amesema ujenzi wa soko jipya eneo la Bondeni kwenye wadi yake unaoelekea kukamilika itasaidia kupiga jeki uchumi wa akina mama eneo hilo mbali na kubadilisha uchumi na maisha ya jamii zao.