BAADHI YA SHULE WADI YA CHEPARERIA ZIMESALIA NYUMA KIMAENDELEO KUTOKANA NA UKOSEFU WA FEDHA


Wadau mbali mbali katika kaunti hii ya Pokot magharibi wetakiwa kujitokeza na kufadhili miradi katika shule mbali mbali katika wadi ya Chepareria eneo bunge la Pokot Kusini.
Mwakilishi wadi wa eneo hilo Patrick Lokomol aidha ameitaka serikali kuharakisha kutoa fedha za kufanikisha maendeleo katika wadi ili kusaidia katika kushughulikia hali hiyo.
Aidha Lokomol ameitaka idara ya elimu kushughulikia swala la upungufu wa walimu hasa wa chekechea katika shule za eneo hilo akisema wale ambao wametumwa kufikia sasa katika shule hizo hawatoshelezi mahitaji ya shule hizo.