ATWOLI ASUTWA BARINGO KUFUATIA KAULI YAKE KUHUSU RUTO


Baadhi ya viongozi katika kaunti ya Baringo wamemsuta katibu mkuu wa muungano wa wafanyakazi nchini COTU Francis Atwoli kutokana na kauli yake kwamba naibu rais Dkt William Ruto anaweza kujitia kitanzi iwapo atapoteza kwenye kinyang’anyiro cha urais.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Bartabwa Ruben Chepsongol viongozi hao wamesema kuwa kwa muda sasa Atwoli amekuwa akionyesha dharau kwa naibu rais na hata kumkosea heshima.
Chepsongol aidha amewakosoa viongozi waliokuwa kwenye mkutano wa jumatatu katika kaunti ya Mombasa ambapo Atwoli alizungumza kwa kusalia kimya na kuonekana kufurahia matamshi yake.
Chepsongol amemtaka katibu huyo wa COTU kutathmini maneno yake anapoongea kwenye mikutano ya hadhara huku pia akielezea imani kwamba naibu rais Dkt Ruto atatwaa wadhifa wa urais.