ASILIMIA KUBWA YA WAKAZI TRANS NZOIA WAKABILIWA NA UHABA WA MAJI LICHA YA KUWEPO VYANZO VYA MAJI.
Imebainika kwamba asilimia 50 ya wakazi wa kaunti ya Trans nzoia hawajasambaziwa maji licha ya kuwa na vianzo viwili vya maji vikiwamo vya mlima Elgon na kile cha Cherangany.
Waziri wa maji na mazingira Aggrey Chemonges amesema takwimu hizo zinatokana na juhudi za kaunti hiyo kuongeza idadi ya wanaopata maji safi na salama kutoka asilimia kumi na nane hadi asilimia 50 tangu ujio wa ugatuzi.
Chemonges amesema kuwa mradi wa kiptogot kolongolo, ukikamilika utazinufaisha familia takriban laki mbili.
Serikali hiyo vilevile inalenga kutumia teknolojia ya zamani kusambaza maji kutoka mto kisawai kwa zaidi ya wakazi elfu tano.