ASILIMIA KUBWA YA WAKAZI TRANS NZOIA HAWANA BIMA YA NHIF.


Imebainika kwamba asilimia 77 ya wakazi wa kaunti ya Trans nzoia hawajajitokeza kusajili kupata bima hivyo basi kutatizika wanapotafuta matibabu .
Akipokea ada ya NHIF kutoka kwa usimamizi wa Transnational times sacco kugharamia matibabu ya wagonjwa wapatao 20 kwa kipindi cha mwaka mmoja, afisa mkuu wa afya wa kaunti hiyo Sammy Masibo amesema tangu kuripotiwa kwa janga la corona wakenya wengi wameshindwa kulipa ada ya hiyo ya NHIF.
Afisa wa mauzo wa trasnational times sacco Tom Nang’endo amesema kwamba takriban shilingi milioni tatu zimewekezwa ili kuwanufaisha wagonjwa kwa muda wa miaka mitatu ijayo.