ASILIMIA 80 YA WANAFUNZI KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI TAYARI WAMEREJEA SHULENI KWA MUHULA WA PILI


Wazazi wametakiwa kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wamerejea shuleni kwa muhula wao wa pili baada ya likizo ndefu ya korona.
Wakizungumza katika shule ya Upili ya wasichana ya Nasokol baada ya kuzizuru shule kadhaa katika kaunti ya Pokot Magharibi, katibu mkuu wa wizara ya Leba Peter Tum na mwenzake wa Teknolojia na Mawasiliano Jerome Ochieng’, wamesema inafurahisha kuona kwamba wanafunzi zaidi ya asilimia themanini katika kaunti nzima ya Pokot wamerejea shuleni kwa muhula wa pili.
Peter Tum ametumia fursa hiyo kuziagiza idara za usimamizi wa shule zote kwenye kaunti hii kuhakikisha kuwa angalau wanafunzi zaidi ya asilimia tisini wameripoti shuleni kufikia wiki ijayo.