ASILIMIA 76 YA WANAUME KAUNTI YA TRANS NZOIA WAMEAMBUKIZWA VIRUSI VYA CORONA


Asilimia 76 ya wanaume kwenye kaunti ya Trans Nzoia wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.
Hii inadaiwa ni kutokana na sekta ya uchukuzi kuwa kizingiti kikubwa kwenye kukabili maambukizi ya virusi hivyo.
Waziri wa afya kwenye kaunti hiyo Clare Wanyama ameyasema hayo.
Wanyama aidha ameongeza kuwa ukosefu wa maji yanayotiririka, kutovalia barakoa na kuchukua viwango vya joto mwilini pia vimechangia kwa ongezeko la maambukizi hayo miongoni mwa wakaazi wa kaunti hiyo.

[wp_radio_player]