ANG’ELEI APUUZILIA MBALI MADAI KUWA AMEJIUNGA NA CHAMA CHA KUP.


Mwakilishi wadi ya Batei katika kaunti hii ya Pokot magharibi Solomon Ang’elei amepuuzilia mbali madai kuwa ni mwanachama wa chama cha KUP kinachoongozwa na gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo pamoja na mbunge wa pokot kusini David Pkosing.
Ang’elei amesema kuwa alichaguliwa kupitia chama cha Jubilee na sasa yeye ni mwanachama wa chama cha UDA kinachoongozwa na naibu rais William Ruto baada kujitenga na chama hicho cha Jubilee.
Ang’elei amesisitiza kuwa atawania tena kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu kupitia tiketi ya chama cha UDA kufuatia kile amesema kuwa chama hicho kina umaarufu mkubwa katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Hata hivyo Ang’elei amesema kuwa hamna tofauti zozote baina ya viongozi wa chama cha UDA na kile cha KUP kwani wote walichaguliwa kuwahudumia wakazi wa kaunti hii, japo akisistiza hamna ushirikiano wa kisiasa baina ya vyama hivyo viwili.