ANC CHAPATA PIGO BUNGOMA MIKONONI MWA UDA.


Chama cha ANC chake Musalia Mudavadi kimepata pigo baada ya mwenyekiti wa chama hicho tawi la kaunti ya Bungoma Johnathan Baraza kugura chama hicho na kujiunga na chama cha UDA kinachoongozwa na naibu rais William Ruto.
Baraza ambaye amehudumu katika wadhifa huo kwa miaka miwili sasa amesema kuwa amechukua hatrua hiyo baada ya majadiliano ya kina na wakazi ambao walimshauri kujiunga na chama cha UDA anachosema kina umaarufu mibwa maeneo ya mashinani ikilinganishwa na ANC.
Akizungumza baada ya kumpokea Baraza, Mshirikishi wa UDA kaunti ya Bungoma Mike Malomba ameipongeza hatua hiyo akisema kuwa chama hicho kinaendeleza majadiliano na viongozi mbali mbali kuhakikisha kuwa kinapata wafuasi wengi kabla ya uchaguzi mkuu.
Aidha Malomba amewahakikishia wafuasi wa chama hicho kuwa kitakuwa na mchujo ulio huru kwa wagombea wake waote.