AMOS WAFULA AMEKABIDHIWA TIKETI NA CHAMA CHA FEDERAL KUWANIA UCHAGUZI MDOGO WA KABUCHAI


Chama cha Federal kimemkabidhi Amos Wafula tiketi ya kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Kabuchai.
Ni rasmi kwamba chama hicho kitawasilisha muwaniaji wake katika uchaguzi huo mdogo wa Kabuchai baada ya Amos Wafula kukabidhiwa tiketi ya chama hicho hafla ambayo iliandaliwa eneo la Msese.
Akizungumza na wanahiabari baada ya kupokezwa tiketi hiyo, Wafula amewataka wakaazi wa eneo hilo kumpa nafasi ya kubadili hali yao kimaisha na kwenye uchaguzi huo.
Akihutubu kwenye hafla hiyo kinara wa chama hicho Andrew Kutitila amewataka viongozi wa eneo hilo vilevile kaunti kwa ujumla kuendesha siasa ambazo anazitaja kama za amani huku akitoa hakikisho kwa wafuasi kuwa chama hicho kitanyakua ushindi kwenye uchaguzi huo.
Kauli Kutitila imeungwa mkono na mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Bungoma na ambaye pia ni mwakilishi wadi Akirim Mlongo.