ALIYEKUWA SPIKA WA BUNGE LA KAUNTI YA TRANSNZOIA AKOSOLEWA VIKALI
Mgombea kiti cha useneta Kaunti ya Trans Nzoia kwa chama cha ODM Muliro Musoke amekosoa vikali hatua ya aliyekuwa Spika Wa Kaunti ya Trans Nzoia Joshua Werunga kuendelea kukosoa utendakazi wa Gavana Khaemba kwa kile amesema ni mmoja wa viongozi ambayo wamechangia pakubwa kudoroa kwa miradi ya maendelo Kaunti hiyo kwa kukosa kutekeleza wajibu wake na wakilishi wadi kwa mujibu wa katiba.
Akihutubu eneo bunge la Cherangani Musoke amesema Werunga ambaye pia anawana kiti cha useneta kwa chama cha DAP K anafaa kuwaelezea wenyeji wa Trans Nzoia jinsi fedha za umma zilivyotumika kwa zaidi ya miaka 4 alipohuduma kama spika kabla ya kuomba nafasi nyingine ya useneta.