ALIYEKUWA MEYA WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI ASHTUMU UONGOZI WA GAVANA JOHN LONYANGAPUO

Viongozi wa matabaka mbali mbali katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendeleza shutuma dhidi ya serikali ya gavana wa sasa John Lonyangapuo kufuatia utendakazi wake katika kipindi cha miaka mitano ambayo ameongoza kaunti hii.

Aliyekuwa meya wa kwanza katika kaunti hii mzee Jacob Samuli amesema serikali ya gavana Lonyangapuo imetoa huduma duni kwa wakazi sekta muhimu kama vile ya afya zikitelekezwa pakubwa huku wakazi wakihangaika kutafuta huduma za matibabu.

Samuli amewataka wakazi wa kaunti hii kuwa makini katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti na kuwachagua viongozi ambao watahakikisha huduma bora kwa mwananchi.

Aidha Samuli amedai kwamba maafisa katika serikali ya gavana Lonyangapuo wamekuwa wakitekelezea majukumu yao katika mazingira magumu.