AKINA MAMA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAHIMIZWA KUJIUNGA KWENYE MAKUNDI ILIKUWEZA KUJIENDELEZA SIKU ZA USONI

Akina mama katika kaunti ya Pokot magharibi wametakiwa kujitokeza na kujiunga na shirika la Joyfull Women Organization ili kuekeza kwa ajili ya kuboresha maisha yao.
Akizungumza na akina mama hao mjini makutano mwanzilishi wa shirika hilo mkewe Naibu wa Rais Rachael Ruto amesema lengo la shirika hilo ni kuwainua akina mama kibiashara huku akidokeza kuwa kufikia sasa amezuru kaunti 46 nchini kuwahamasisha akina mama.
Aidha bi. Ruto amewataka akina mama hao kujiunga na vikundi na kujisajili ili kuekeza na kuanza kupokea mikopo ya biashara zao
Kwa upande wake, Meneja wa shirika hilo la Joywo Julius tanui anasema kiwango cha chini zaidi cha kuekeza ni shilingi 200 pekee fedha ambazo amesema akina mama wengi wanaweza kumudu
Hata hivyo baadhi ya wanachama wakiongozwa na Pamela Sigei wametaka shirika hilo kuchukua jukumu la kuwawezesha akina mama kibiashara haswa wale ambao hawana ajira ili kuwafaa zaidi