AKINA MAMA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KUNUFAIKA NA MRADI WA USHANGA


Serikali kuu itashirikiana na serekali ya kaunti hii ya pokot magharibi kuhakikisha kuwa kina mama ambao wanajihusisha na shughuli ya kushona na kuuza ushanga wananufaika na biashara hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shughuli ya kutoa mafunzo kwa kina mama wanaojihusisha na biashara hiyo, waziri wa michezo na utamaduni amina mohammed amesema kuwa serikali pia itahakikisha kina mama hao wanatafutiwa soko kwa jili ya bidhaa zao.
Waziri wa utamaduni, utalii, michezo na vijana kaunti hii joel arumonyang ambaye alikuwa ameandamana na waziri amina amesema kina mama takriban 450 katika kaunti hii watanufaika kwenye mpango huo.
Kina mama ambao wanajihusisha na biashara hiyo wamepongeza serikali kwa kuzindua mpango huo wanaosema utakuwa wa manufaa makubwa kwao ikizingatiwa biashara hiyo ndiyo tegemeo lao kiuchumi.