AFISI YA WATOTO MJINI KAPENGURIA YAWAONYA WALE AMBAO WANAENDELEZA UKEKETAJI NA KUWAOZA WATOTO WA KIKE KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Afisa katika idara ya watoto mjini Kapenguria Fredrick Nyatigi amesikitishwa na visa vya ukeketaji na kuwaoza wasichana mapema katika kaunti ya Pokot Magharibi.
Nyatigi amewaonya vijana wanaohusika katika kuwalazimisha mabinti hao kuoleka na kuwalazimu kusitisha masomo yao.
Akizungumza ndani ya Kalya Radio Nyatigi ameelezea kuwa kuwaoza na kuwakeketa wasichana kunaathiri zaidi maisha yao ya usoni.
Wakati uo huo Nyatigi amewataka washikadau wote katika jamii kushirikiana na serikali katika kukomesha dhuluma kwa watoto wa kike kwa kuwaripoti wahalifu watakaopatikana wakijihusisha na ukeketaji, kuwaoza mapema, ubakaji miongoni mwa dhuluma nyingine katika jamii.