AFISI YA USAJILI WA WATU TRANS NZOIA YATAKIWA KUHARAKISHA ZOEZI LA UTOAJI VITAMBULISHO.
Wito umetolewa kwa afisi ya usajili wa watu kuharakisha mchakato wa kutoa vitambulisho kwa vijana ili ili wapate nafasi ya kujisajili kuwa wapiga kura kwenye awamu ya pili ya usajili wa wapiga kura inayoendelezwa na tume ya uchaguzi na mipaka IEBC.
Wakiongozwa na Shadrack Kimtai Chemalima ambaye ametangaza nia ya kuwania kiti cha ubunge eneo la Cherangan kaunti ya Trans nzoia, viongozi hao wamesema vijana wengi wanakosa stakabadhi hiyo muhimu itakayowawezesha kujisajili kuwa wapiga kura, akitoa wito kwa wale ambao hawajachukua vitambulisho vyao kuvichukua katika afisi za chifu.
Wakati uo huo Chemalima ametoa wito kwa umma kujitokeza kwa wingi na kujisajili kuwa wapiga kura ili kushiriki uchaguzi mkuu wa Agosti 9, kwa kuwachagua viongozi watakaobadilisha uongozi, siasa na maendeleo eneo bunge la Cherangani.