AFISI YA ARDHI YA KAUNTI YA TRANS NZOIA YASHTUMIWA KUTOKANA NA UFISADI


Viongozi katika kaunti ya Trans Nzoia wameilaumu pakubwa afisi ya ardhi katika kaunti hiyo wakisema kuwa imekuwa kizingiti katika kutoa vyeti vya umiliki wa ardhi.
Viongozi hao wakiongozwa na kiongozi wa Kiboroa Squatters Association Ineah Masinde, wamedai afisi hiyo imejaa ufisadi wakisema huenda hali hiyo ikalemaza pakubwa ajenda nne kuu za rais Uhuru Kenyatta anayehudumia kipindi chake cha mwisho.
Kauli ya viongozi hao hata hivyo imetiliwa mkazo na mwakilishi wadi ya Keiyo Emmanuel Waswa ambaye pia ametaka kufanyiwa mabadiliko afisi hiyo ili kuwapa wenyeji huduma bora.