AFISA WENGINE WAWILI WAMERIPOTIWA KUFARIKI KATIKA ENEO LA KAPEDO


Mkuu mwingine wa polisi na dereva wake wamethibitishwa kuuawa baada ya kupigwa risasi na washukiwa wa ujambazi katika eneo la jana jioni.
Mshirikishi wa utawala katika eneo la bonde la ufa George Natembeya ambaye amethibitisha kisa hichi amesema kuwa kamanda wa polisi anayesimamia kitengo cha polisi wa kushughulikia hali za dharura RDU alivamiwa pamoja na dereva wake ambaye pia ni polisi katika daraja la Amiyan eneo bunge la Tiaty ambapo raia mmoja pia alijeruhiwa kwenye tukio hilo.
Natembeya aidha amesema kuwa mkuu huyo wa polisi anayesimamia kambi za Lomelo na Kapedo alikuwa anarejea kazini baada ya kuhudhuria mazishi ya mamake.
Wakaazi wa eneo hilo hata hivyo wamelalamika utovu wa usalama ambao umekithiri.