AFISA WA POLISI AMPIGA RISASI MWANAMKE MMOJA KACHELIBA KUFUATIA MZOZO WA KIMAPENZI.


Mwanammke moja kutoka soko la kacheliba kaunti ya Pokot Magharibi anauguza majeraha ya risasi tumboni baada ya kupigwa risasi na afisa mmoja wa polisi asubuhi ya jumatatu.
Inadaiwa afisa anayejulikana kama Isaac osome alimfytetulia risasi hiyo wakiwa pamoja na afisa wa kaunti ndogo ya kongelai almaarufu D.E.O alitoka kituo cha Kongelai eneo bunge la Kapenguria.
Kwa sasa maafisa wa dci wanafanya uchunguzi katika eneo hilo ambako mwanammke huyo alipigiwa risasi huku afisa huyo akizuiliwa katika kituo cha polisi cha Kapenguria.
Inaiwa kwamba afisa huyo alichukua aumuzi huo kufuatia mzozo wa kimapenzi.
Mwanammke huyo alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Kapenguria ambako anaendelea kupokea matibabu kufuatia majeraha aliyopata kutokana na risasi hiyo.