VIONGOZI BONDE LA KERIO WAAHIDI KUSHIRIKIANA KUKABILI UJANGILI

Viongozi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wameahidi kushirikiana na wenzao wa kaunti jirani ya Elgeyo marakwet katika juhudi za kuhakikisha kwamba kunashuhudiwa amani ya kudumu maeneo ya mipakani pa kaunti hizi mbili.

Wakizungumza eneo la Kapushen katika hafla ya mazishi ya vijana wawili waliouliwa, kamologon na majangili, viongozi hao wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Weiwei David Moiben wamesema watahakikisha wahalifu wanaotekeleza mauaji hayo wanapatikana na kukabiliwa vilivyo.

Aidha viongozi hao wamewataka wakazi wa kaunti hii kutolipiza kisasi kufuatia tukio hilo na badala yake kuwaachia viongozi kwa ushirikiano na wazee pamoja na maafisa wa usalama kushughulikia swala hilo la usalama.

Kwa upande wao ujumbekutoka kaunti ya Elgeyo Marakwet wakiongozwa na waziri wa vyama vya ushirika Robert Kangogo wametaka kambi ya jeshi kujengwa eneo la Kamologon pamoja na kujengwa barabara za eneo hilo ili kuimarisha hali ya usalama.