SOKO LA KISASA KUJENGWA ENEO BUNGE LA SABOTI

TRANS NZOIA


Wenyeji wa wadi Tuwani eneo bunge la Saboti kaunti ya Trans-Nzoia wanatazamia kufaidi kupitia kwa ujenzi wa soko la kisasa kwa ushirikiano wa serikali kuu na serikali ya kaunti kwa kima cha shilingi milioni 55.
Akihutubu kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo mwakilishi wadi wa Tuwan Bernard Wambua amesema hatua hiyo itasaidi kipiga jeki uchumi wa wenyeji wa mabanda eneo hilo mbali na kutoa nafasi bora ya kufanya biashara kwa wenyeji eneo hilo, akiwaonya walionyakua ardhi ya umma kuondoka kwenye ardhi hizo ili kutoa nafasi ya utekelezwaji wa miradi ya serikali.
Kwa upande wake afisa mkuu wizara ya ardhi, mipango na ujenzi kaunti ya Trans-Nzoia Bi Susan Ngera na menaja wa manispaa ya Kitale Patrick Nyongesa wamepongeza hatua hiyo wakisema itapiga jeki uimarishaji wa ukusanyaji wa ushuru na kuinua uchumi wa kaunti hiyo mbali na kuondoa msongamano wa wanabishara katikati ya mji wa kitale.
Mwakilishi wa wizara ya nyumba na ujenzi Bi Irine Gikera amesema soko hilo litakuwa na vibanda 120 huku msaidizi wa kamishana kaunti ya Trans-Nzoia Timaah Ali Omar akitoa wito kwa mwanakandarasi kuajiri vijana kutoka mtaa huo.