MBUNGE WA POKOT KUSINI AONYWA DHIDI YA KUMHARIBIA JINA GAVANA WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi Simon Kachapin ameendeleza shutuma dhidi ya mbunge wa Pokot kusini David Pkosing kwa kile amesema kwamba kutumia vyombo vya habari kumharibia jina.

Akizungumza jana katika maadhimisho ya siku ya jamhuri yalioandaliwa katika uga wa Makutano, Kachapin amemtaja mbunge huyo kuwa kiongozi anayendeleza siasa za kiwango cha chini badala ya kutumia muda wake kuwashughulikia wakazi wa eneo bunge lake.

Kachapin amewataka viongozi wa kaunti hii kujitenga na siasa za migawanyiko na kushirikiana katika kuwatendea kazi wananchi, akiahidi kushirikiana na viongozi wote bila kuzingatia miegemeo ya vyama vya kisiasa ili kuhakikisha wananchi wanapokea huduma hitajika.

Wakati uo huo Kachapin amesema kwamba sasa serikali yake iko tayari kuanza kuwahudumia wakazi wa kaunti hii baada ya kujaza nafasi mbali mbali ikiwemo mawaziri na makatibu wa wizara mbali mbali akiwahakikishia wananchi kuanza rasmi kupokea huduma za serikali.