WAZAZI BARINGO WALAUMIWA KWA KUWAFICHA WANAO WENYE ULEMAVU.

Wazazi katika kaunti ya Baringo wametakiwa kutowaficha wanao walio na changamoto ya ulemavu na badala yake wawasajili katika idara za serikali ili kuhakikisha kwamba wanashughulikiwa ipasavyo.

Akiongea mjini kabarnet mkurugenzi wa idara ya vijana na jinsia katika serikali ya kaunti ya Baringo Daudi Aengwo  alisema kuwa baadhi ya wazazi, na walezi waliwaficha watoto walemavu wakati wa zoezi la hesabu ya watu mwaka 2019.

Aengwo aliwataka wazazi na pia jamii kwa ujumla kufahamu kwamba watoto walemavu wana haki sawa na wenzao wasio na changamoto zozote zile za kimaumbile.

“Wazazi na walezi waliwaficha watu wanaoishi na ulemavu wakati wa sensa. Mzazi anapasa kuelewa kwamba mtoto au mtu yeyote mwenye ulemavu ni mtu kama mwingine na hamna mtu ambaye alipenda kuwa mlemavu.” Alisema Aengwo.

Aengwo aliongeza kuwa kutokana na idadi ndogo iliyonakiliwa ya watu wenye changamoto ya ulemavu, kaunti hiyo haijakuwa ikipokea ufadhili wa kutosha kutoka serikali kuu na wahisani.

“Hatungeweza kuwashawishi wafadhili kuuunga mkono kaunti ya Baringo kutokana na idadi ndogo ya watu wenye ulemavu iliyoandikishwa katika kaunti hii. Hatuwezi pia kupata ufadhili wa kutosha kutoka kwa serikali ya kaunti na ya kitaifa kutokana na idadi hii ndogo.” Alisema.

Mkurugenzi huyo sasa anawataka maafisa wa serikali kuu kwa ushirikiano na watawala wa wadi yani ward administrators kushirikiana ili kuendesha zoezi la kubaini idadi kamili ya walemavu katika kaunti hiyo.

“Tunaomba wasimamizi wa wadi kuchukua idadi kamili ya watu wanaoishi na ulemavu, na kunakili aina ya ulemavu alio nao mtu ili anagalau tupate ufadhili kwa ajili ya watu wetu wenye ulemavu.” Alisema.