MAAFISA WA POLISI WAKASHIFIWA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KWA KUWEKA VIZUIZI KWENYE BARABARAKUU YA LODWAR KITALE

Mbunge wa kapenguria Samuel Moroto amesema inasikitisha kuona kwamba kaunti ya pokot magharibi ina zaidi ya vizuizi 15 vya barabarani kutoka mji wa makutano hadi sigor na maeneo mengine, Vituo ambavyo viko kinyume cha sheria na vinatumika kuwanyanyasa Wahudumu wa magari.

Moroto amesema ni sharti vizuizi hivyo viondolewe Barabarani na wahudumu wa Magari kuwachwa huru kwani Polisi hutumia vituo hivyo kuitisha hongo kutoka kwa wananchi.

Wakti uo huo, mbunge huyo amewataka polisi wanaoshika doria katika mji wa makutano na kwengineko kutowahangaisha wakaazi kwenye sehemu za burudani iwapo maeneo hayo ya biashara yana Leseni na yanahudumu kihalali,

Naibu Gavana  Robert Komole  amewataka Maafisa wa Usalama kutoka kaunti za Baringo,Pokot Magaribi,Turkana na Marakwet kushirikiana wakati wanaendesha oparesheni katika kaunti hizo.

Aliposimama kutoa Hotuba yake Gavana Kachapin amesema aliandaa kikao na kaunti kamishna na kuwataka mafisa wa usalama kutowahangaisha wafanyibiasha sehemu mbali mbali kaunti ya Pokot magharibi.

Hata hivyo kaunti kamishna anasema anahitaji ushirikiano na viongozi walio chaguliwa ilikuakikisha wanafanikisha upatikanaji wa maendeleo.