WAZIRI ALIYEAPISHWA KAUNTI YA POKOT AAHIDI KUHAKIKISHA HALI ZA HOSPITALI ZOTE ZINAIMARIKA

Waziri wa afya katika kaunti hii ya Pokot magharibi Cleah Parklea amewaahidi wakazi wa kaunti hii huduma bora na sawa za afya katika hospitali na zahanati zote zinazopatikana katika kaunti hii chini ya uongozi wake kwenye idara hiyo.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa rasmi kuhudumu katika idara ya afya, Parklea aidha amesema kwamba atazingatia uagizaji mapema wa dawa kutoka shirika la kusambaza dawa na vifaa vya matibabu KEMSA ili kukabiliuhaba wa dawa katika vituo vya afya kaunti hii.

Wakati uo huo Parklea ameahidi kuhakikisha kwamba dawa na vifaa ambavyo vinaagizwa kutumika katika hospitali na vituo mbali mbali vya afya kaunti hii vinatekeleza majukumu hitajika na wala si kutwaliwa na wahudumu wa afya katika hospitali hizo.