IDADI YA WENYEJI KUNGATWA NA NYOKA YAONGEZEKA KAPTARA BARINGO
Jumla ya visa 378 vya watu kung’atwa na nyoka vimeripotiwa katika maeneo tofauti ya kaunti ya baringo kati ya mwezi januari na septemba mwaka huu 2022, huku idadi kamili ya vifo ikikosa kubainika wazi.
Akiongea kwenye kijiji cha kaptara katika eneo bunge la baringo ya kati wakati wa hafla ya kuwahamasisha wakazi kuhusu hatua za kufuata mtu anapong’atwa na nyoka, afisa mkuu wa idara ya mifugo dr. Winnie bore amesema kuwa idadi hiyo ni iliyosajiliwa hospitalini.
Dr bore amesema kuwa huwenda watu zaidi wameumwa na nyoka kwani kuna uwezekano kwamba baadhi ya waathiriwa hawakutafuta huduma za matibabu kwenye vituo vya afya.
Kwa upande wake chifu wa lokesheni ya lelmen joshua kipseree amesema kuwa jumla ya watu 6 wameaga dunia baada ya kuumwa na nyoka wenye sumu kali ambao huonekana kwa wingi wakati wa kiangazi.
Kwa upande wao jacob chelimo ambaye ni mmoja wa eneo hilo ameitaka serikali ya kaunti kuhakikisha kwamba inasambaza dawa ya kukabili sumu ya nyoka yaani anti venom kwenye vituo vya afya ili kuzuia maafa ya watu.