UHABA WA MUKOMBERO WAKUMBA MAGHARIBI YA NCHI.

Uhaba wa mukombero unakumba eneo la Magharibi mwa Kenya na kuwalazimu wafanyabiashara kuvuka mpaka na kuingia taifa jirani la Uganda kusaka mmea huo.

Wafanyabiashara wa mukombero sasa wanahofia kwamba katika miaka michache ijayo, mmea huo ambao ni dawa ya kupunguza mfadhaiko utatoweka.

Kulingana na Simon Ondula, ambaye ni mchuuzi wa mukombero mjini Kakamega, mmea huo ulianza kupungua msituni kutokana na uvunaji ulioachwa watu wasio wataalamu.

Ondula anasema watu hao wasiokuwa na ujuzi wa kuvuna mukombero hung’oa kila kitu ardhini bila kuacha sehemu ya nyingine ya mumea huo kuchupika upya.

Anaeleza kuwa hiyo imewalazimu wakulima wa mukombero kupanda mimea ya kuiga kwenye mashamba yao ili kukabiliana na uhaba.

Alisema mmea huo unaonja tofauti hivyo wateja ni wachache.

“Watu hawaipendi sana, na kutulazimisha kwenda katika msitu wa Kamuli nchini Uganda kwa mali asili ya dawa hiyo ambayo inauzwa sana.”

“Nchini Uganda uvunaji unadhibitiwa, watu wanavuna kwa ajili ya biashara, si matumizi ya nyumbani. Nadhani hiyo ndiyo sababu ya udhibiti,”alisema Ondula