WAAKILISHI WADI TRANS NZOIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA GAVANA NATEMBEYA.


Viongozi wa kidni katika kaunti ya Trans nzoia wamewataka waakilishi wadi katika kaunti hiyo kushirikiana na gavana George Netembeya na kuhakikisha kuwa wanapitisha miswada muhimu ili kuiwezesha kaunti hiyo kuimarika kimaendeleo.
Wakiongozwa na askofu Raymond Mutama, viongozi hao waliwataka waakilishi wadi kutofuata mkondo wa watangulizi wao ambao wamedai kuwa walimpa wakati mgumu gavana wa kwanza wa kaunti hiyo Patrick khaemba awamu ya kwanza ya ugatuzi.
Aidha viongozi hao wamewataka viongozi katika kaunti hiyo kuweka kando tofauti zao za kisiasa na badala yake kushirikiana ili kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.
“Tulishuhudia hali ngumu sana wakati gavana Khaemba alianza kazi. Alikuwa na waakilishi wadi wachache mno upande wake. Na tumeona swala hili limerudia tena wakati huu wa gavana Natembeya kwani ana waakilishi wadi wachache upande wake.” Alisema Mutama.
Aliongeza kwa kusema, “Sisi kama viongozi wa kidini tunaweka mikakati ya kumfikia gavana pamoja na waakilishi wa wadi ili kuwahimiza kufanya kazi pamoja. Maswala ya uchaguzi yalikamilika na sasa tunachohitaji ni maendeleo.”
Wakati uo huo viongozi hao wamemtaka gavana Natembeya kufanya kipau mbeke vita dhidi ya ufisadi wanaosema umechangia pakubwa kaunti hiyo kusalia nyuma kimaendeleo.
“Yule gavana tuliyekuwa naye alizingirwa na watu wafisadi ambao hawakumsaidia. Na sasa gavana aliyepo sasa ni lazima ajihadhari kwani wale walaghai bado wapo.” Walisema.