CHAGUZI ZA UBUNGE POKOT KUSINI NA KACHELIBA ZAAHIRISHWA.


Uchaguzi maeneo bunge ya kacheliba na Pokot kusini katika kaunti hii ya Pokot magharibi umesitishwa.
Kulingana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati uamuzi huo uliafikiwa kufuatia mkanganyiko kwenye karatasi za kupigia kura kwenye maeneo hayo.
Chebukati amesema kuwa karatasi za kupigia kura za wagombea katika wadhifa huo zilikuwa na picha zisizo sahihi.
Aidha Chebukati ametangaza kusitishwa uchaguzi wa ugavana katika kaunti za kakamega na Mombasa kwa sababu zizo hizo.
Chebukati amesema kuwa tarehe ya uchaguzi wa maeneo hayo itatangazwa hapo baadaye.
Hatua hiyo imeshutumiwa vikali na waathiriwa wakisema kuwa ni njama ya kuathiri kura zao.
Wakiongozwa na mwaniaji wa ugavana kaunti ya Kakamega Cleophas Malala na mbunge wa Suna mashariki junet Mohammed wagombea hao hata hivyo wametaka wafuasi wao kujitokeza kwa wingi kuwachagua viongozi wao.