IEBC YAENDELEZA MAANDALIZI YA UCHAGUZI SIKU 6 TU KABLA UCHAGUZI WA AGOSTI 9.


Siku 6 tu kabla ya uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi huu wa agosti, tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeendelea kuweka mikakati ya awamu za lala salama kwa maandalizi ya uchaguzi huo wa juma lijalo.
Akizungumza na kituo hiki afisa wa uchaguzi katika tume hiyo kaunti ya Pokot magharibi Joyce Wamalwa amesema kuwa kwa sasa wanashughulikia swala la mtandao katika maeneo ambako kuna tatizo la mtandao akiwahakikishia wakazi kuwa upeperushwaji wa matokeo hautaathirika na hali hiyo.
Aidha Wamalwa amesema kuwa tume hiyo itatumia magari spesheli kusafirisha mitambo ya kupigia kura katika maeneo ambako kuna tatizo la usafiri kufuatia hali mbovu ya barabara.
Kwa upande wake afisa katika afisi ya msajili wa vyama vya kisiasa Lorta Erukudi amesema afisi hiyo inashirikiana na tume ya IEBC pamoja na vyama vya kisiasa ili kuhakikisha kunakuwepo amani kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi huo.