MASHIRIKA YA KIJAMII YABUNI JUKWAA LA KUKABILI MIMBA ZA MAPEMA POKOT MAGHARIBI.


Visa vya mimba za mapema miongoni mwa watoto wa kike wenye umri mdogo vimeendelea kuripotiwa nchini hasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi wengi wa watoto wa kike wakishindwa kuendelea na masomo yao.
Ni kutokana na hali hii ambapo shirika la DSW kwa ushirikiano la lile la baya yalibuni jukwaa kwa jina Life yangu kwa lengo la kuwahamasisha vijana kuhusu umuhimu wa kudhibiti mfumo wao wa afya ya uzazi hasa kupitia matumizi ya vifaa au tembe salama za kuzuia mimba.

Kulingana na Ann Wangacha, afisa wa mawasiliano katika shirika la DSWhatua ya kubuniwa jukwaa hili pia ilichochewa na changamoto ambayo ilitolewa na serikali kupitia wizara ya afya kwa wadau kubuni mbinu ambazo zitasaidia kukabili mimba za mapema miongoni mwa watoto wa kike.

Ni kauli ambayo imesisitizwa na afisa wa miradi katika shirika hilo Masika Mwinyi ambaye aidha amesema kuwa mashirika hayo yalikumbatia matumizi ya mtandao kuwahamasisha vijana kutokana na hali kuwa katika dunia ya sasa wengi wa vijana wanatumia muda wao mwingi mitandaoni.