RAIS KENYATA ASUTWA KWA UTOVU WA MAADILI.


Mbunge wa kapenguria katika kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto amemsuta vikali rais Uhuru Kenyatta kwa kile amesema kutoonyesha maadili yanayofaa kwa kiongozi wa hadhi yake kinyume na walivyofanya watangulizi wake.
Akizungumza na wanahabari mjini makutano Moroto amesema kuwa kinyume na watangulzi wake, rais Kenyatta pamoja na maafisa wanaohudumu katika serikali yake wamehusika pakubwa katika majibizano na taasisi nyingine za serikali ambazo zinaonekana kwenda kinyume na matarajio yake.
Moroto ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakenya wote kuendelea kuishi kwa umoja na kudumisha utulivu licha ya joto la kisiasa kuonekana kupanda nchini wakati huu ambapo taifa linakaribia uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Wakati uo huo Moroto amekariri madai kuwa machifu wanashinikizwa kuunga mkono mwaniaji urais wa chama cha muungano wa azimio la umoja one Kenya Raila Odinga, akiwataka kutokubali shinikizo hizo kutoka kwa serikali na badala yake kutekeleza majukumu yake kulingana na katiba.