RAILA AAHIDI KUSHUGHULIKIA UTOVU WA USALAMA KERIO VALLEY.
Mgombea urais wa muungano wa azimio Raila Odinga ameahidi kuweka mikakati ya kuimarisha usalama kwenye kaunti za Pokot magharibi, Baringo Elgeyo marakwet na Turkana iwapo atachaguliwa rais katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Akizungumza jumatano katika misururu ya kampeni kwenye kaunti za Pokot magharibi, Baringo na Elgeyo Marakwet, Raila alisema kuwa anafahamu tatizo la usalama ambalo linashuhudiwa maeneo haya ambayo chanzo chake kikuu ni wizi wa mifugo.
Raila aliahidi kujenga viwanda vya kutumia mazao ya kutoka shambani katika kaunti hizi pamoja na kaunti zingine ambazo pia zinakumbwa na tatizo la usalama na ambako kilimo kinaweza kufanya vyema.
Aidha Odinga aliwahakikishia wakulima wa mahindi kwamba serikali yake itafanya kipau mbele ununuzi wa mahindi kutoka humu nchini na kwamba serikali ya azimio itanunua tu mahindi kutoka nje ya nchi iwapo wakulima watakosa kuzalisha mahindi ya kutosha kukidhi mahitaji ya maelfu ya wakenya.
Aliweka wazi kuwa serikali yan azimio itapunguza bei ya mbolea kutoka shilingi alfu 6 hadi shilingi alfu 2 ili kuimarisha sekta ya kilimo.