WAFANYIKAZI TRANS NZOIA WARIDHIA HATUA YA SERIKALI KUTOA BIMA.


Mwenyekiti wa muungano wa wafanyakazi wa serikali ya kaunti ya Trans Nzoia Samuel Juma Kiboi amepongeza hatua ya serikali ya Kaunti hiyo kutoa bima ya afya kwa wafanyakazi kaunti hiyo akisema hii ni hatua nzuri ya kutoa hakikisho la afya bora kwa wahudumu hao.
Kwenye mkao na wanahabari mjini Kitale Kiboi amesema  hatua hiyo itasaidia wafanyakazi kaunti hiyo kupunguza gharama ya juu ya matibabu kila wakati wakiwa wagonjwa mbali na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Wakati huo huo Kiboi amemtaka  gavana Patrick Khaemba kuhakikisha  serikali yake inalipa deni la shilingi milioni 59 ilizoamriwa na mahakama baada ya kishinda kesi iliyohusu kufutwa kazi wafanyakazi mwaka wa 2002, mbali na kuwaajiri wafanyakazi ambao wamehudumu kwa kandarasi kwa zaidi ya  miaka 10.