SENETA WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AMETOA WITO KWA WAKAAZI WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KUWA MAKINI WANAPOPIGA KURA
Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio ametoa wito kwa makundi ya kina mama, vijana na walemavu kuwa makini katika uchaguzi mkuu wa mwezi agoti katika wadhifa wa mwakilishi kina mama na kumchagua mgombea ambaye atahakikisha kuwa maswala yao yanangaziwa vyema.
Akizungumza na kituo hiki Poghisio amesema kuwa ni wakati makundi hayo yanapasa kufanya mabadiliko katika uongozi wa wadhifa huo kwa kumchagua mwakilishi kina mama mpya baada ya kushuhudia uongozi wa wagombea wawili wa wadhifa huo ambao tayari wamewahi kuhudumu katika wadhifa husika.
Poghisio amempigia debe mgombea kiti hicho kupitia chama cha KANU ambaye ni spika wa bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi Catherine Mukenyang akimtaja kuwa kiongozi ambaye yuko katika nafasi bora ya kuwahudumia wakazi kutokana na tajriba yake katika uongozi kaunti hii.